Jumatano , 15th Jun , 2016

Klabu ya Simba imefanikiwa kumnasa kiungo wa Mtibwa Sugar Muzamil Yassin kwa Mkataba wa miaka miwili huku ikiendelea kuhaha kutafuta saini ya kiungo mwingine wa timu hiyo Shizza Kichuya.

Muzamil anakuwa mchezaji wa tatu kusaini Simba, baada ya beki Emmanuel Semwanza na kiungo Jamal Mnyate wote kutoka Mwadui ya Shinyanga.

Wengine ambao Simba inahaha kukamilisha usajili wao ni Salum Meshack Kimenya na Jeremiah Juma wote wa Tanzania Prisons.

Dirisha la usajili kwa vilabu vyote shiriki vya Ligi limefunguliwa rasmi leo ambapo linatarajiwa kufungwa Agosti 06 mwaka huu.