Jumatano , 1st Jun , 2016

Bendi ya Mapacha Watatu iliyokuwa ikiundwa na msanii Josse Mara pamoja na Khalidi Chokoraa imesambaratika baada ya msanii mmoja wa bendi hiyo kujitoa na kuelekea kurudi katika bendi yake ya awali Twanga Pepeta.

Wasanii waliounda Bendi ya Mapacha Watatu Khalidi Chokoraa,Jose Mara na Chalz Baba.

Akizungumza na eNewz Jose Mara alisema kuwa kwa sasa katika bendi hiyo amebaki peke yake baada ya kuondoka kwa wasanii wenzake Chalz baba pamoja na Chokoraaa na kwa sasa bendi hiyo imebadili jina inafahamika kwa jina la New Mapacha Watatu.

Pia Chokoraa aliiambia eNewz kuwa yeye ametoka mapacha watatu kutokana na kipato kuwa kidogo ukilinganisha na hali ya maisha yake hawezi kubaki katika bendi hiyo kwa sifa tu ya kuwa humo yeye alichokifanya ni kujiongeza baada ya kupata sehemu yenye kipato cha zaidi.

“Ni utafutaji wa maisha tu lakini hakuna kitu kingine chochote mimi nikiwa kama binadamu mwenye akili timamu nimejitambua nimeona kwamba hapa kuna haja ya kubadilisha upepo,” alisema Chokoraa.