Jumanne , 22nd Apr , 2014

Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu nchini Tanzania NIMR, imesema kuwa inaanza kufanya tafiti za kubaini kama kuna tishio lolote la ugonjwa wa Ebola hapa nchini.

Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu - NIMR, Dkt Mwele Malecela

Hayo yameelezwa na mkurugenzi mkuu wa NIMR Dkt Mwele Malecela leo jijini Dar-es-salaam wakati akielezea matayarisho ya kongamano la sayansi la taasisi ya taifa ya magonjwa ya Binadamu litakaloanza kesho jijini Dar-es-salaam.

Kwa mujibu wa Dkt. Malecela Tafiti hizo za kubaini uwepo wa magonjwa ya mlipuko kama ebola utaanza mara tu baada ya Taasisi hiyo kupata Maabara inayohama au Mobile Laboratory kwa ajili ya shughuli hizo, maabara inayotarajiwa kufika nchini hivi karibuni ikwa ni maabara ya pili ya aina hiyo barani Afrika nyingine ikiwa nchini Nigeria.