Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego,
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika shule ya msingi Madimba, mkurugenzi wa shirika hilo, James Mataragio, amesema mchango huo unatokana na shirika hilo kutambua na kutekeleza kwa vitendo dhana ya uwajibikaji kwa jamii hasa zile ambazo shughuli za utafiti na uendelezaji wa gesi na mafuta zinafanyika na zile zinazopitiwa na miundombinu ya gesi.
Aidha, sambamba na mchango huo, shirika hilo limekabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. Milioni 150 kwa halmashauri hiyo, ikiwa ni malipo ya tozo za huduma (Service levy) kwa shughuli za uzalishaji na uchakataji wa gesi.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, ameushukuru uongozi wa shirika hilo kwa mchango huo na kusema kuwa halmashauri ya wilaya ya Mtwara ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madawati kama ilivyo kwa halmashauri nyingine nchini.