Ijumaa , 1st Apr , 2016

Wazee na viongozi wa vijiji mkoani Njombe wametakiwa kuwaunganisha vijana wao na ushirika ili kujitengenezea mazingira ya kukopesheka kirahisi na kurithi miradi waliyoianzisha wazee wao miaka ya nyuma.

Baadhi ya wakulima na wawakilishi wa vyama vya ushirika Njombe (Picha na Maktaba).

Kauli hiyo imetolewa na Mrajisi vya Vyama vya Ushirika mkoa wa Njombe, Jafeth Sapali baada ya kubainika kuwa kuna wazee wengi kwa zaidi ya asilimia 90 wako kwenye vyama hivyo, huku vijana wengi wakiogopa kujiunga na ushirika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Matembe, Amcos Clamence Malekela, amesema kuwa elimu inahitajika ili kuwavutia vijana kujiunga na ushirika katika kujiletea maendeleo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Matembe, Bryson Malekela na wazee wanatoa suluhisho la kitu kitakacho wavutia vijana kujiunga na ushirika ni pamoja na bodi kupita vitongoji kwa vitongoji na kuwapa elimu na ushauri vijana hao juu ya umuhimu wa ushirika.

Hata hivyo vijana wanaeleza kitu kinacho wakwaza kujiunga na ushirika licha ya wazazi wao kuwa ni wanaushirika kuwa ni masharti mengi ambayo kwao wanahisi ni magumu lakini pia na kutumia majina ya zamani katika ushirika huo kunawakosesha kuweza kujiunga.

Vyama vya ushirika vilianzishwa miaka ya nyuma na kuwasaidia wananchi wa miaka hiyo kabla ya kusimama kwa muda na kuanza tena hivi karibuni kwa kufufua miradi yake na wazee ambao walikuwa ni vijana wa zamani kuonekana wengi kuliko vijana.