
Waziri wa maendeleo ya Nishati na Madini nchini Uganda, Irene Muloni
Ujio wa Waziri huyo ambao umepokelewa na maafisa kutoka wizara ya nishati na madini, umetokana na maamuzi yaliyofikiwa kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, uliofanyika jijini Arusha mwezi February Mwaka huu.
Akizungumza katika ziara hiyo katibu mkuu wa wizara ya Nishati na Madini Prof. William Mtarikwa, amesema kuwa licha ya kupata upinzani kutoka kenya juu ya ujenzi wa bomba hilo lakini Tanzania ina nafasi kubwa zaidi ya kutekeleza mradi huo kushinda Kenya.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela amesema kuwa serikali ya Tanzania ipo tayari kuanza mradi huo mara moja huku Mkuu wa bandari ya Tanga, Henri Arika akisema usalama wa bandari ya Tanga ni mkubwa kushinda bandari nyingine yoyote.
Mradi huo utakapo kamilika utasaidia zaidi kupanua fursa za kiuchumi kwa mkoa wa Tanga na kuongeza pato la Mkoa huo na Tanzania nzima kwa Ujumla.