Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa TNGP mtandao Bi.Lilian Liundi
Kaimu mkurugenzi mtendaji wa TNGP mtandao Bi. Lilian Liundi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na East Africa na kuwataka viongozi wa serikali na vyama washirikiane katika kutatua kero za wananchi bila ubaguzi wa kiitikadi ili kuleta mabadiliko nchini na kupunguza umaskini.
Bi. Lilian amesema kuwa ucheweleshwaji wa uchaguzi ikiwemo ya Mameya unarudisha nyuma maendeleo na waathirika zaidi wa migogoro hiyo ni wananchi kwa kuwa wanakaa bila ya viongozi ambao wanatakiwa kuwatatulia kero zao na kuwaletea maendeleo.
Pia Bi. Lilian amewataka viongozi waliopewa dhamana waweze kutatua migogoro yao kwa ustaraabu bila ya fujo wala kukashifiana kwa kuwa wananchi wanahitaji zaidi maendeleo kuliko malumbano yanayoletwa na viongozi hao.
Aidha mkurgenzi huyo ameitaka serikali ya awamu ya tano iendelee kuwachukulia viongozi wanaokwenda kinyume na tarabu kwa kuwawajibisha kulingana na matakwa ya kazi yanavyoelekeza bila kubagua katika hatua hizo za kinidhamu.
Katika hatua nyingine Bi. Lilian amekemea kitendo cha udhalilishaji alichofanyiwa Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam ambaye kwa siku hiyo ya uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam alikuwa anakaimu Ukurugenzi Wa Jiji Bi Theresia Mmbando.