Ommy Dimpoz
Kuhusiana na kazi hii mpya ambayo picha zake zimekwisha onekana mitandaoni, Dimpoz ameweka wazi kuwa imekuwa ni somo kubwa kwake kufanya kazi hii iliyo katika kiwango cha kimataifa, akiwa chini ya uongozaji wa mtayarishaji video mkubwa kabisa, Moe Musa ambaye anafanya kazi zake huko Uingereza.
Ommy Dimpoz amesema kuwa, kutokana na kiasi cha pesa ambacho amewekeza katika video hii, muda na kufuatilia mpangilio wa ratiba ya kazi bila kuweka utani, kazi hii itaacha gumzo hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla pindi itakapotoka.