Jumatano , 9th Apr , 2014

Serikali ya Tanzania imeanza kushughulikia ripoti ya Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch ambayo imedai kuwa idadi kubwa ya watoto nchini wamekuwa wakifanyishwa kazi kinyume na sheria
za kimataifa ambazo nchi imeziridhia.

Kamishna wa kazi kutoka Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Saul Kinemela, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa mpango wa kitaifa wa kukabiliana na tatizo la ajira kwa watoto wadogo.

Bw. Kinemela amefafanua kuwa serikali inafahamu jinsi watoto wanavyofanyishwa kazi katika maeneo kama ya migodi, kuomba omba na kufanya biashara ndogondogo barabarani, na kwamba kwa kiasi kikubwa
ripoti ya Human Rights Wacht ilikuwa na ukweli.