Waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), akikagua ujenzi wa Daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo jijini Dar es salaama mara baada ya ziara ya kukagua ujenzi wa barabara katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam
Prof. Mbarawa amewasihi wakandarasi kuendelea na kazi ya kumalizia ujenzi huo kwa kuwa serikali iko katika mchakato wa kuwalipa huku akiwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati fidia zao zikiendelea kushughulikiwa.
Ziara hiyo ya waziri Mbarawa ilianzia Mbezi Tangi Bovu kupitia Goba, Mbezi Kimara, Tabata Kinyerezi, Ukonga Majumba sita, Tabata Dampo kupitia Kigogo.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa wakala wa barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale amesema changamoto ya mradi huo ni pamoja na uhaba wa fedha za fidia na malipo kwa wakandarasi.
Barabara za mlisho zina jumla ya urefu wa kilometa 27. 2 na zitajengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi bilioni 56. 3.