Mhe. Temba
Mhe. Temba ambae anaunda kundi la TMK Familly akiwa anashirikia pia kwa ukaribu na Chege, amesema kuwa alilazimika kununua fanicha za ndani kutokana na mauzo ya album hiyo, ambapo aliweza kubadili hata maisha ya nyumba ya familia aliyokuwa anaishi.
Temba amesema wakati anaingia katika muziki shagazi yake ambae ndie alikua mlezi wake, alikua hataki kabisa yeye kujihusisha na muziki lakini baada ya kubadilisha nyumbani kwa album hiyo, ndio milango yake kwenye game ikafunguka.