Jumatatu , 1st Feb , 2016

Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe.Zitto Kabwe ameiomba serikali kupitia Bunge lake la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuacha kufanya kazi kwa matakwa ya watanzania wachache na kuwaacha watazania wengi ambao ni walipa kodi kwenye mamatizo.

Ameyasema hayo mjini Dodoma alipokuwa akizungumza na East Africa Radio wakati akifafanua kile kinachoendelea kwa sasa Bungeni na kuwaomba wabunge wenzake kuhakikisha wanasimamia haki ya kikatiba katika kutafuta maendeleo ya nchi na kuongeza pato la taifa.

Amesema kuwa watanzania wengi wanategemea wawakilishi wao ambao ni wabunge waliowachagua kidemokrasia kuwafikishia matatizo yao serikali kupitia Bunge kwa lengo la kuwasaidia na kuyatatua matatizo yao ndani ya kijamii zao.

Aidha Mhe. Zitto amesema kuwa haipaswi bunge kubanwa kitu ambacho kitaminya demokrasia, hivyo ni vyema bunge likaachiwa huru lifanye kazi yake ya kuisimamia serikeli kama sheria na kanuni inavyotaka.

Msikilize hapa;-