Klabu ya Manchester United huenda ikawa klabu itakayokuwa ikipokea pesa nyingi zaidi duniani katika kipindi cha miezi 12 ijayo.
Kwa mujibu wa orodha ya mapato ya klabu iliyotayarishwa na kampuni ya Deloitte, miamba wa Uhispania Real Madrid kwa sasa wanaongoza kwa mwaka wa 11 mfululizo ambapo katika msimu wa 2014-15 iliingiza euro milioni 577 zaidi ya shilingi za kitanzania Trilioni 1.4.
Mabingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Barcelona wanashikilia nafasi ya pili wakiwa na euro milioni 560.8 zaidi ya Trilion 1.3 huku United wakiwa nambari tatu kwa kujipatia euro milioni 519.5 zaidi ya trillion 1.2.
Lakini Deloitte wamesema kuna uwezekano mkubwa sana kwamba United huenda wakawa wamewapita Real Madrid wakati wa kutolewa kwa orodha ijayo.
Kwa mujibu wa Deloitte, “ukuaji thabiti wa kibiashara” wa Manchester United, pamoja na “uwezo wa kupata mikataba ya thamani kubwa ya uthamini” kama ule wa Adidas wa paund milioni 75 kila mwaka, vimesaidia kwa kiasi kikubwa klabu hiyo.
Manchester United ilishuka kutoka nambari mbili hadi nambari tatu baada ya kushuka kwa mapato yao, jambo ambalo Deloite imesema linaweza kuchangia United kuipita Real Madrid.