Naibu waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina.
Naibu waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema hayo katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Morogoro ambapo kutokana na ukiukwaji huo wa sheria za mazingira kiwanda cha sukari cha Ilovo kimetozwa faini ya sh.mil 25 kutokana na kuwa na mfumo mbovu wa utunzaji wa taka ngumu na kushindwa kuhifadhi vyema mabaki ya mabati na kutakiwa faini hiyo ilipwe ndani ya siku saba na kurekebisha changamoto hizo.
Aidha Mhe. Mpina amesema kiwanda cha ngozi cha Ace waliotakiwa kudhibiti harufu mbaya inayolalamikiwa na wakazi,wao wametakiwa kulipa mil.15 kwa kuwa na mfumo mbovu wa utiririshaji na uhifadhi maji taka.
Katika ziara yake kwenye soko kuu la mjini Morogoro Naibu waziri huyo ametaka ujenzi mpya wa soko hilo kuzingatia vizimba vya uhifadhi wa taka ili zisitawanyike, na kutofanyika milundikano ya muda mrefu ya taka katika eneo hilo.