Alhamisi , 14th Jan , 2016

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu hiyo imemnunua kiungo wa kati wa FC Basel Mohamed Elneny.

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kwamba klabu hiyo imemnunua kiungo wa kati wa FC Basel Mohamed Elneny.

Mchezaji huyo anaweza kucheza kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza dhidi ya Stoke Jumapili.

Elneny, 23, anaripotiwa kuwagharimu Gunners £5m na anaweza kucheza katika Ligi ya Klabu Bingwa barani Ulaya baada ya kupata vibali.

Uhamisho wa kiungo huyo wa Misri ulichelewa baada ya Arsenal kuangaikia vibali vya kufanya kazi nchini Uingereza, na kukamilika kwa uhamisho huo inakuwa usajili wa kwanza kwa washika mitutu hao kwenye dirisha dogo la mwezi Januari.

Elneny amechezea timu ya taifa ya Misri mara 39 na kufunga mabao 3 ni mchezaji anayecheza kiungo hasa cha ukabaji ambapo atajiaandaa kwenda kugombani namba na viungo wa Arsenal kama Francis Coquelin, Mathieu Flamini na Mikael Arteta katika kiungo cha ukabaji.