mwanasoka wa Tanzania Mbwana Samatta aliyetwaa Tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika wa CAF
Wadau mbalimbali wakiwepo wasanii wa muziki wamempongeza nyota huyo wa kambumbu na kutoa maoni yao kuhusiana na mafanikio hayo.
Staa wa muziki ambaye pia ni mcheza soka, H-Baba ameongea na eNewz kuhusiana na ushindi wa mwanasoka huyo na kusema kuwa, nidhamu ndio kitu cha pekee kilichomsaidia kufika alipo, akilaumu wachezaji wengi wa Tanzania kutumia vilevi na kuendekeza starehe zinazowapoteza.
Kwa upande wa Madee ambaye ni mdau mkubwa wa soka akieleza kuwa rekodi nzuri ya Samatta ilimhakikishia ushindi wake,naye mwigizaji na msanii mahiri nchini Dokii, katika kuguswa na ushindi huo wa Samatta hakubaki nyuma, ameingia studio na kutengeneza rekodi kwa ajili ya Mbwana Samatta.