
Mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Towmn Kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga, amechomwa moto na dada yake Esther Julius,kwa kuwaeleza marafiki zake aliokuwa anacheza nao kwamba hua anabakwa na shemeji yake.
Tukio hilo limetokea juzi nyumbani kwao katika mtaa wa Majengo kata ya Kambarage baada ya dada huyo kusikia kutoka kwa marafiki wa mtoto huyo wakieleza kusikia kutoka kwa mwenzao kwamba hua anabakwa na shyemeji yake aliyejulikana kwa jina la Pius Julius na kumfanya mtoto huyo kubakia na majeraha mdomoni na kwenye mashavu.
Jirani wa nyumba hiyo Mariam Ally alisema kuwa alisikia sauti ya mtoto huyo akilia kwa sauti na alipotoka nje aligundua alikuwa ameunguzwa kwa moto na akasikia watoto wenzake wakielezea jinsi alivyowaambia kuwa hua anabakwa na shemeji yake,tukio hilo lilimfanya awapigie simu polisi ambao walifika na kumtia nguvuni dada huyo.
Kwa upande wa mtoto huyo alieleza kufanyiwa kitendo hicho mara kwa mara wakati wa usiku dada huyo akiwa hayupo na alipomwambia dada yake alikuwa akimtishia kumpiga endapo atatoa siri hiyo.
Mtuhumiwa bado anashikiliwa na jeshi la polisi na shemeji yake anaetuhumiwa kubaka alifanikiwa kutoroka wakati mtoto huyo amepatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa na kuruhusiwa kuondoka .