Jumapili , 27th Dec , 2015

Rapa kutoka mkoa wa Mbeya Izzo Bizness amekiri kuwa mwaka huu umekuwa wenye mafanikio kwake katika game ya muziki akiweka wazi kuongeza idadi kubwa ya mashabiki pamoja na kufanya kolabo mbalimbali za wasanii kama staa wa muziki Navio wa Uganda.

Rapa anayeuwakilisha mkoa wa Mbeya Izzo Bizness

Izzo ambaye ametoa pongezi kubwa kwa kituo maarufu cha Televisheni cha East Africa TV kwa kuweza kuzitangaza kazi za wasanii nchini, amesema EATV imewasaidia kwa kiasi kikubwa kupata mashavu ya kufanya kazi na wasanii nje ya Tanzania.