Ijumaa , 25th Dec , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri ya Sikukuu ya Krismasi watanzania huku akisisitiza kuendelea kushikamana na kufanya kazi kwa bidii.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri ya Sikukuu ya Krismasi watanzania huku akisisitiza kuendelea kushikamana na kufanya kazi kwa bidii.

Magufuli ametoa ujumbe huo katika Ibada ya Sikukuu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu iliyofanyika katika kanisa katoliki la mtakatifu Petro, Oysterbay Jijini Dar es Salaam alipo hudhuria misa ya kwanza katika kanisa hilo.

Naye Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kardinali Pengo amesema amefurahishwa na ushiriki wa Rais katika misa hiyo na kumkaribisha atoe salamu kwa watanzania

Akizungumza mara baada ya kukaribishwa, Dkt.Magufuli amewatakia heri ya Sikukuu ya Krismasi watanzania wote na kuwataka kushikamana..

Kwa upande mwingine,Rais Magufuli amewataka watanzania kuiombea serikali ya awamu ya tano ili iweze kutimiza majukumu ya kitaifa na kwa ufanisi mkubwa.

Katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Azania Front jijini Dar es salaam, katika Ibada ya Krismas, Msaidizi wa Askofu wa Kanisa hilo Mchungaji Chadiel Lwiza amesema kuongezeka kwa migogoro nchini ikiwa ni pamoja ya wakulima na wafugaji ni kutokana na kukosekana kwa upendo nchini.

Ibada hiyo Kitaifa, imefanyika Kitaifa katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Anthony wa Padua Jijini Tanga.