Alhamisi , 3rd Apr , 2014

Miss Tanzania, mrembo Happines Watimanywa, amesema kuwa, tangu amelitwaa taji hilo kubwa la urembo hapa nchini mpaka sasa, kitu ambacho kinamgusa sana kukifanya ni namna ambavyo anapata nafasi ya kukutana na wanafunzi na kuzungumza nao.

Happiness Watimanywa, Miss Tanzania 2013-14

Happiness amesema kuwa, anafurahia sana wakati huu kutokana na kuweza kuwashauri na kuwapa muongozo wanafunzi hawa, juu ya namna ya kufikia katika malengo yao, kitu ambacho huwasaidia kubadilisha maisha yao kwa namna moja ama nyingine.

Kwa upande mwingine pia, eNewz tukazungumza na Happiness kuhusiana na suala zima la mapenzi na iwapo yupo kwenye mahusiano kwa sasa, ambapo mwanadada huyu amesema kuwa ana mpenzi wake na hangependa kumuweka hadharani kwa sasa.