Ijumaa , 18th Dec , 2015

Rapa Witnesz anatarajia kumaliza mwaka na zawadi kubwa kwa mashabikiwa wake, video ya rekodi yake ya 'Buku Jero' ambayo amejipanga kuizindua rasmi leo usiku katika shoo kali ya Friday Night Live.

Rapa Witnesz aka Kibonge Mwepesi

Witnesz amesema kuwa, kazi hiyo imekuwa na visa kibao nyuma yake mpaka kukamilika kwake, ikiwa pia ni uwekezaji mkubwa ambao hata hivyo amegoma kuweka wazi thamani yake akihofia kuwatisha wasanii wenzake katika gemu kama anavyoeleza hapa.