
Akitangaza albam hiyo mwenyekiti wa RIAA Cary Sherman, amesema hiyo ni mara ya kwanza kwa msanii kufika 30X platnum, na wanaheshima kubwa kusherehekea jambo hilo lililoweka historia kwenye muziki.
“RIAA imezawadiwa rekodi ya dhahabu na platinum kwa niaba ya biashara ya muziki takriban miaka 60, lakini hii ni mara ya kwanza kwa msanii kufikisha 30X multi-platinum, tuna heshima kubwa kusherehekea hadhi hii ya Thriller kwenye historia, ni hatua ya kipekee na alama ya kudumu kwenye mioyo yetu na historia ya muziki,” alisema Cary Sherman.
Thriller ni albam ya kwanza kuwahi kuuza kopi milioni 30 nchini Marekani, na kuuza kopi milioni 100 dunia nzima, na ilipotoka iliingia kwenye tuzo za grammy mara 12 na kushinda mara saba, pia ilikaa namba 1 kwa wiki 37 katika chati za Billboards.
“Hii inathibitisha kwamba Michael Jackson ni msanii bora wa muda wote, sio kwa nyimbo zake na mauzo yake tu kupiga hatua, bali muziki wake ulikuwa wa dunia, Thriller ilikuwa sahihi, ninajivunia kwamba Michael ni moyo na nafsi ya Epic Records na milele atabaki kuwa mfalme peke wa Pop”, aliendelea kusema mwenyekiti wa Shirikisho hilo.
Michael Jackson amefariki mnamo tarehe 25 Juni 2009 baada ya kuwaisha katika hospitali ya UCLA Medical baada ya kupata mshtuko wa moyo, uliotokana na matumizi mabaya ya madawa mengi.
