Kikosi cha zamani cha Mtibwa Sugar kilichotamba msimu uliopita
Akizungumza na East Africa Radio msemaji wa wakatamiwa hao Thobius Kifaru amesema kikosi chao kipo imara na wachezaji wapo katika hali nzuri ya kiushindani hivyo wamepania kuvuna alama zote tatu muhimu mbele ya Mbeya City.
Kifaru ametamba kikosi chao kitaendeleza kasi waliyoanza nayo msimu huu ambapo mpaka ligi inakwenda mapumziko wakata miwa hao wa Manungu wameshinda saba, wakitoka sare mmoja na kufungwa moja na kushikilia nafasi ya tatu kwa pointi zao 22 nyuma ya Vinara Azam wenye ponti 25 na Yanga walio kwenye nafasi ya pili kwa ponti zao 23.
Mtibwa chini ya kocha wao Meky Mexime watakunana na Mbeya City iliyo chini ya Meja Abdul Mingange ambaye ana kazi ya ziada ya kuitoa kwenye nafasi ya 11 kwa pointi zao 10.