Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Said Mecky Sadiki akifanya Usafi chini ya Daraja la Jeshi lililopo Mlalakuwa. Picha na maktaba
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Said Mecky Sadiki amewataka wakazi wa jiji Dar es Salaam kujitokeza kufanya usafi hapo kesho kama ilivyotangazwa na Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa siku ya Uhuru Desemba 9, itumike kufanya usafi badala ya kusherehekea vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.
Akiogelea utaratibu wa zoezi hilo hapo kesho, Bw. Sadiki amesema wenyeviti wa serikali za mitaa wanawajibika kusimamia zoezi hilo litakaloanza mapema saa kumi na mbili asubuhi na kupeleka taarifa ya utekekezaji wa agizo hilo ili kuchukua hatua ambao wamekiuka kufanya usafi.
Bw. Sadiki amesema maandalizi ya zoezi hilo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa mbalimbali huku akiwataka wakuu wa wilaya,kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa,watendaji na wenyeviti wa serikali ya mtaa kushirikiana kufanikisha usafi katika maeneo yao..