Jumatatu , 7th Dec , 2015

Kufuatia kutoka kwa rekodi ya 'Hili Game' iliyokuwa inangojewa kwa hamu kubwa kutoka kwa rapa mkongwe katika game ya Bongofleva, Jay Moe siku ya leo, staa huyo ameongea na eNewz kufafanua ujumbe mzima ambao ameamua kuwasilisha kupitia kazi hiyo.

rapa mkongwe katika game ya Bongofleva, Jay Moe

Aidha Jaymoe ameoonekana kuponda baadhi ya mambo ambayo yanaonekana kuwa ni hatua ambazo muziki wa kizazi kipya umepiga kufika hapa ulipo.

Jay Moe amesema, amelazimika kugusia mambo hayo, ikiwepo uwekezaji mkubwa katika video za wasanii kuliko rekodi, uwepo wa mameneja katika game kati ya mambo mengine, akiamini kuwa kuna nafasi ya kubadili baadhi ya mambo ili maendeleo ya muziki wa Tanzania yakae katika njia sahihi.