Ijumaa , 4th Dec , 2015

Klabu ya Mbeya City imefanikiwa kuwasajili wachezaji wawili mlinzi wa kati Tumba Sued kutoka Coastal Union na Aliyekuwa Mshambuliji wa Toto Africans Abdallah Juma kati ya watano ambao wamepanga kuwaongeza katika usajili huu wa dirisha dogo.

Mkuu wa Mbeya City Emmanuel Kimbe amesema, wamemsajili Tumba ili kuchukua nafasi ya Juma Nyosso ambaye amefungiwa kucheza mpira kwa miaka miwili.

Kimbe amesema, wanaendelea na mazungumzo na wachezaji wengine ambao mwalimu amewapendekeza kuwasajili lengo likiwa ni kuongeza wachezaji watano kufikia tarehe 15 mwezi huu siku ambayo usajili utafungwa.

Kimbe amesema, kikosi kinashuka dimbani Desemba 13 kucheza dhidi ya Mtibwa Uwanja wa Sokoine ambapo tayari kikosi kipo kambini kwa wiki ya pili huku wakiwa wamedhamiria kufanya vizuri zaidi baada ya ligi kuanza tena baada ya kusimama kwa miezi karibia miwili.