Jumamosi , 28th Nov , 2015

Kili Stars itashuka dimbani Jumatatu kupambana na wenyeji Ethiopia katika mechi ya robo fainali ya michuano ya kombe la CECAFA Chalenji.

Wakati Stars imeingia robo fainali kama kinara wa Kundi A, Ethiopia imetumia ‘mlango wa uani’ maarufu kama best looser baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Stars leo.

Bao la Kill Stars lilifungwa na Mshambuliaji wake Simon Msuva dakika ya 52 huku Ethiopia ikijipatia bao lake la kusawazisha kupitia bao la kujifunga kutoka kwa Beki Salim mbonde wa Kill Stars na kupelekea matokeo kuwa sare ya moja kwa moja.

Mechi hiyo ya Jumatatu inatarajiwa kuwa ngumu kwa kuwa Ethiopia ambao wameonesha wazi hawana kikosi imara, watakuwa wameongeza hali ya kujiamini baada ya sare hiyo iliyowavusha hadi robo fainali huku Stars ikiingia robo fainali baada ya kushinda mechi zote mbili na kutoa sare moja katika hatua ya makundi.

Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Kili Stars, Abdallah Kibadeni amesema ana imani na kikosi chake kwani kilicheza vizuri na anaamini mechi itakuwa ngumu kwa kuwa wapinzani wao wapo nyumbani kama wenyeji, lakini watapambana kwa kuwa wametumwa na watanzania