Jumatano , 25th Nov , 2015

Nyota wa muziki aliyejijengea jina akiwa na kundi la watu Pori, Koba MC ambaye amebadili kwa kiasi kikubwa mahadhi ya muziki anayofanya, hivi sasa ameamua kusimama katika mitindo ya mchiriku na mdundiko.

Nyota wa muziki kutoka kundi la Watu Pori, Koba MC

Mkali huyo ambaye ni mkazi wa mkoani Morogoro amesema ameamua kufanya mabadiliko ya kuingia zaidi katika miondoko hiyo kutokana na wasanii kutambua ladha na utajiri wa mahadhi ya muziki kutoka hapa nyumbani.

Koba ameieleza eNewz kuwa, njia ambazo amerejea nazo hazitofautiani na kule ambapo amepita Chegge Chigunda, Nay wa Mitego kati ya wengine, ikiwa pia ni kwenda sambamba na kile ambacho wengi walitamani kuona, wasanii wa hapa nyumbani wakijivunia na kufanya muziki ambao una asili ya hapa na kuacha kuiga mataifa mengine.