Akizungumza jijini Dar es salaam wakati akitoa mwelekeo wa hali ya kisiasa pamoja na mchakato wa katiba mpya, mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Deus Kibamba amesema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania shughuli za Bunge haziathiriwi na kuwepo au kutokuwepo kwa wawakilishi kutoka Zanzibar kutokana na kutofanyika uchaguzi.
Kibamba akizungumzia Katiba Mpya amesema ufanyike mchakato wa ukamilishaji wa katiba mpya ili kufanya mageuzi katika utendaji kwa serikali kama aliyoaanza kwa kufanya ziara katika taasis za serikali na kuharakisha uwajibikaji kwa viongozi wa umma kutokana na kuwa na misingi katika katiba
Akizungumzia hali ya Zanzibar, Mwanasheria wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Harold Sungusia akizungumzia utata uliopo wa kuruhusiwa Dk. Ali Shein kuingia bungeni kuwa halina athari yoyote kwa mujibu wa sheria.
Amesema kwa mujibu wa Ibara 95 kuwa kutokuwepo kwa wabunge 25 wa baraza la wawakilishi hakubatilishi uhalali wa shughuli za bunge na kuwa kama Rais anayemaliza muda wake katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ataalikwa ana haki ya kuhudhuria.