Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania aliemaliza muda wake Bi. Anne Makinda
Bi. Makinda ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akiongea na waandishi na kuongeza kuwa wabunge wengi wakimaliza muda wao hupata shida kwani hawana pensheni tofauti na watumishi wengine wa serikali au sekta binafsi.
Bi Makinda amesema kuwa watu wengi wana dhana kuwa wabunge wana fedha nyingi tofauti na hali halisi ambayo wako nayo wabunge hao na hayo yanadhihiri pindi wanapokosa au kustaafu Ubunge.
Aidha Spika huyo anayemaliza muda wake amesema kuwa Spika mpya lazima awe Mvumilivu kwa kuwa bunge lina mchanganyiko wa wabunge tofauti na hivyo linahitaji kiongozi mwenye busara, hekima ili kuisimamia na kuishauri vizuri serikali.
Katika hatua nyingine Bi. Makinda amesema kuwa anapumzika na hataki nafasi yoyote ya uongozi baada ya kuhudumu kwa muda mrefu akiwa kama mbunge wa jimbo la Njombe kusini pamoja na kuwa spika wa bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.