Jumanne , 3rd Nov , 2015

Klabu ya Simba SC imewapa mapumziko mafupi ya siku 17 wachezaji wake wakati huu ambao Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara imesimama kwa muda.

Kocha mkuu wa kikosi hicho, Muingereza Dylan Kerr amesema amewapa mwongozo wachezaji wa timu hiyo juu ya namna ya kujitunza katika kipindi hiki.

Kerry amesema, amewapa likizo fupi wachezaji ingawa hawaendi kupumzika kabisa, kwani kila mmoja amepewa maelekezo juu ya nini cha kufanya kila siku na watakaporudi kila mmoja atafanya jaribio kulingana na maelezo yaliyopo kwenye karatasi.

Kerr amesema mazoezi ambayo wanakwenda kuyafanya wakiwa katika kipindi hiki cha mapumziko ni mazoezi ya viungo zaidi.

Ligi kuu imesimama kupisha maandalizi ya timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo Novemba 14 mwaka huu itakuwa na mechi mbili za kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Algeria na itakaporejea mchezo wa kwanza wa Simba SC utakuwa dhidi ya vinara wa ligi, Azam FC.