Jumatatu , 19th Oct , 2015

Rapa Jua Cali kutoka nchini Kenya amegusa nyoyo za wengi baada ya kutembelea kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu huko Kibera nchini Kenya, na kutoa msaada wa nguo, ikiwa ni namna yake ya kurejesha shukrani kwa jamii.

Rapa Jua Cali kutoka nchini Kenya akiwa na watoto wanaoishi katika mazingira magumu

Sambamba na msaada huo, Jua Cali ambaye anaendelea kuyapata katika muziki na biashara zake pia amepata nafasi ya kuzungumza na watoto hawa na kuwapa hamasa, kitendo ambacho kimegusa nyoyo za asilimia kubwa ya mashabiki wake, ikiwa pia ni njia ya kuwajengea moyo watoto hao kutokukata tamaa kwa mwanzo mgumu wa maisha yao.

Jua Cali amekuwa akiendesha zoezi la kufikisha mavazi kwa jamii ambazo zimekuwa na uhaba chini ya mpango wake wa Ng'arisha Initiative ambapo mara kwa mara amekuwa akifanya ziara kama hizi kufikisha misaada kwa walengwa.