Jumapili , 18th Oct , 2015

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe, amesema iwapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza nchi, atahakikisha anajengwa viwanda mbalimbali nchi nzima.

Wagombea Urais wanaochuana vikali katika kinyang'anyiro hicho, Mh. Edward Lowassa na Dkt. John Pombe Magufuli.

Aidha, Rungwe amewataka wananchi kumpigia kura za urais na sambamba na kuwapigia kura wagombea ubunge na udiwani kutoka vyama vingine vya siasa ili kutoa ushindani wa kweli bungeni na katika vyombo mbali mbali vya maamuzi.

Awali, mgombea mwenza wa chama hicho, Issa Habasi Hussein, ametaja vipaumbele vya chama hicho kuwa ni ajira, mikopo isiyo na riba kwa wafanyabiashara wadogo wadogo pamoja na huduma za elimu na afya kuwa za bure.

Kwa Upande wake Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Jijini Mwanza katika viwanja vya Furahisha aliwaambia wakazi wa Jiji hilo kuwa anataka jiji hilo liwe kituvu cha biashara kwa kanda ya Afrika Mashariki.

Nae Mgombea Urais anaeungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kupitia CHADEMA, Mh. Edward Lowassa alishindwa kuwahutbia wakati wa Tunduma kwa kile kilichodaiwa vipaza sauti vibovu hivyo mkutano huo umepangwa kufanyika leo Asubuhi.