Mjumbe wa bodi ya viziwi Tanzania Selina Lema
Mjumbe wa bodi ya viziwi Tanzania Selina Lema amesema kuwa maelekezo mengi yanayotolewa na viongozi wa tume ya taifa ya uchaguzi pamoja na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi yamekuwa yakishindwa kuwafikia kutokana na kukosekana kwa watafsiri wa lugha.
Aidha Bi. Selina ameongeza kuwa hata vyombo vya habari navyo vimeshindwa kufanya hivyo jambo linalotishia uwezekano wa kutokea athari mbalimbali kwa viziwi iwapo watafanya vitu kinyume na matakwa ya tume.
Kwa upande wake mratibu wa mafunzo ya kitaifa ya elimu ya uraia kwa viziwi Stadius Kongoka amesema jamii kubwa ya viziwi imekosa elimu hiyo ya uraia hata baada ya kuzungumza na viongozi na kwamba hawaoni jitihada zozote zinazo fanyika.