Jumamosi , 3rd Oct , 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete amezitaka mamlaka husika zinazohusiana na Usafiri wa barabara kukaa ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili madereva ikiwemo kupata mitakaba ya kudumu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete

Akiongea na madereva katika mkutano waliotumia kumuaga Rais Kikwete amesema kuwa matatizo mengi ya madereva hao yanasababishwa na watendaji waliopewa dhamana ya kuleta maendeleo na usimamizi bora katika sekta hiyo ya usafiri.

Dkt. Kikwete amewataka viongozi wa Sumatra, Wizara ya kazi pamoja na vyama vya madereva pamoja na waajiri kukutana kutoka na maazimio ambayo yatakuwa ni muafaka kwa kila mmoja wao.

Kabla ya mkutano huo Rais Kikwete alizindua jengo la wazazi na watoto katika hospital ya CCBRT Dkt. Kikwete ambapo amesema vifo vitokanavyo na mama kujifungua hapa nchini sasa vimepungua kutokana na idadi ya akina mama wanaojifungulia katika vituo vya afya kuongezeka.

Kwa upande waziri wa afya na ustawi wa jamii nchini Dkt. Seif Rashid amesema takwimu zinaonesha kwamba zaidi ya wakina mama wajawazito laki 5 wanajifungulia kwenye vituo vya afya tofauti na miaka iliyopita.