Submitted by Anonymous on Ijumaa , 28th Mar , 2014 P square wakisalimiana na waandishi wa habari mara walipowasili uwanja wa taifa wa ndege Mwl. Julius Kambarage Intl. Airport, p square wakiwasiliana na mashabiki wake walipowasili uwanja wa ndege. Wasanii wa Bongo wakiwa pamoja na P square mara baada ya kuzungumza na waandishi wa Habari. P square wakiongea na waandishi wa habari siku kabla ya Tamasha P square wakijadiliana jambo na lady Jay D kabla ya kufanya show. Gadner Habash akiwa na wasanii wa kundi la Hip Hop la kizazi kipya la Weusi wakipozi kwa picha ya pamoja. Mtangazaji maarufu wa East Afrika television Dulla akiwa na floor Manager Dickson wakifurahia tamasha. Msanii mkali wa Hip Hop nchini Nikki wa pili akiwa nyuma ya jukwaa akisubilia kupanda kwenye steji. Pro. Jay akiwa na marafiki zake kwenye picha ya pamoja. Vijana wa East Africa Television Dulla na Tbwai 360 wakiwa stejini wakiendeza tamasha la P square live in Dar Ben Paul akifungua steji la burudani kabla ya kuwakaribisha P square. Ben Paul akiumwayamwaya moyo wake na kupagawisha mashabiki waliofika kumshuhudia. P square wakileta burudani mwanana jukwaani huku wakionyesha staili zao maarufu za kudansi. Prof. jay naye akiwakumbusha mashabiki kwamba bado yupo na bado kwa kutoa burudani mwanana. P square wakionyesha ujuzi wakutumia vyombo mbali mbali vya muziki. Mashabiki waliofika kushuhudia tamasha hilo la kufunga mwaka. P square wakiongea na mashabiki katika burudani. Mkali wa Joto hasira Lady jayd akitumbuiza jukwaani na nyimbo zake maarufu. Mashabiki wakisherekea tamasha la P square. Peter wa Psquare akionyesha kufurahishwa hadi kuvua shati kuleta burudani zaidi. peter akiwaimbia kwa hisia mashabiki wake. Mrembo a.k.a beautiful Onyinye aliyepata fursa ya kupanda stejini na kupewa saa ya Peter wakati wa tamasha. Mashabiki wakifurahia tamasha hilo. P square wakionyesha umahiri wwao wakutawala steji na dansi. P square wakiwashukuru mashabiki wao kwa kufika.