Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania chini ya umri wa miaka 19, itakosa michuano ya kriketi ya Afrika kwa mwaka huu, kufuatia mgogoro wa uongozi kwenye chama cha kriketi cha dunia.
Nahodha wa timu ya taifa ya kriketi na kocha wa timu za taifa za mchezo huo, Hamisi Abdalah,amesema hadi sasa hawajapokea taarifa yoyote juu mualiko wa mashindano ya vijana ambayo hufanyika kila mwaka mwezi desemba.
Ameongeza kwa kusema kuwa kila kitu kitajulikana tarehe 10 mwezi ujao kuhusu mgogoro huo, lakini kwa kipindi hiki chama cha kriketi Tanzania kinataraji kuandaa mashindano ya wanawake ya kriketi kwa mikoa mitano ili kuzipa mazoezi timu za wanawake ambazo zimekosa mashindano ya Afrika kwa mwaka huu.




