Jumanne , 22nd Sep , 2015

Star wa muziki Janjaro a.k.a Dogo Janja amefunguka kupitia eNewz kueleza shughuli ambazo anazifanya pembeni ya muziki, hii ikiwa ni kufuatia kimya cha muda mrefu huku mashabiki wakitaka kufahamu ni kitu gani kinaendelea katika maisha yake.

Staa wa muziki Janjaro aka Dogo Janja

Janjaro ambaye amekuwa chini ya usimamizi wa Madee katika kipindi chote hicho, ameeleza kuwa, pembeni ya kazi hiyo ya muziki amekuwa akijiweka karibu na biashara, akionekana pia akijihusisha na matangazo ya mavazi ya wabunifu, binafsi akisema ana nyenzo kadhaa za kumpatia pesa.