Jumanne , 22nd Sep , 2015

Maabara za afya za binafsi na za serikali iwapo zitakuwa bora zitasaidia kutoa mchango mkubwa kufanikisha huduma za kinga na tiba, na kutumika kuweka mipango endelevu ya kutekekeza huduma za afya hapa nchini.

Kaimu msajili wa bodi ya maabara binafsi Dickson Majige.

Akizungumza na wakaguzi wa mikoa wa maabara binafsi za afya nchini, Kaimu msajili wa bodi ya maabara binafsi Dickson Majige, amesema huduma za maabara ndio sehemu pekee inayo wawezesha madaktari kufahamu tatizo la mgonjwa hivyo nivyema kuboresha sekta hiyo ili kuwezesha upatikanaji wa tiba sahihi za kitaalamu zisizo za kubahatisha.

Majige ameongeza kuwa katika kuhakikisha huduma za maabara zinakuwa bora, bodi hiyo imekagua vifaa vilivyoingia nchini kupitia uwanja wa ndege na bandari zilizopo jijini Dàr es salaam na kusajili maabara 151, wauzaji 53 wa vifaa na vitendanishi na kutoa kibali kwa maabara sita kwaajili ya kupima kipimo maalum cha widal test.

Hata hivyo bado tatizo la wamiliki wa maabara kutotambua wajibu wao wa kazi na kuajiri watu wasio na sifa, kuwa na maabara zisizokidhi viwango au kusajiliwa kwa mujibu wa sheria na kutoa majibu yasiyo sahihi kwa wagonjwa, pamoja na matumizi ya vyeti feki, imekuwa kikwazo kikubwa.

Kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo anasema uboreshwaji wa sheria zilizopo utaweza kusaidia kukomesha tatizo hilo na changamoto zingine za maabara.