Jumatatu , 21st Sep , 2015

Msanii wa muziki wa Injili nchini Tanzania, Emmanuel Mbasha ameongea na eNewz kuelezea furaha na shukrani zake baada ya kushinda kesi ya tuhuma za kubaka iliyokuwa ikimkabili kutokana na mkubwa wa kifamilia aliokuwa nao na mkewe.

Msanii wa muziki wa Injili nchini Tanzania, Emmanuel Mbasha

Mbasha akiwa katika furaha kubwa baada ya kuvuka kiunzi hicho kilichokuwa kikimkabili, ameeleza kuwa kwa sasa anaendelea na shughuli zake za muziki kama kawaida, huku akimuachia Mungu suala zima la hatma yake na mkewe ambaye ni dhahiri kuwa maelewano yao bado si mazuri.