Mmoja wa wagombea urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC, Hamad Rashid Hamad ambae alikua ni mmoja ya wagombea waliojitokeza katika mdahalo huo.
Hayo yamesemwa leo mjini Zanzibar wakati wa mdahalo wa wazi uliowakutanisha wagombea wa nafasi za urais kupitia vyama mbalimbali kisiwani humo ambapo wagombea waliohudhuria mdahalo huo kutoka chama cha ADC, Hamad Rashid na CHAUMA, Mohamed Masoud Rashid , ACT-Wazalendo wamesema kushirikiana kwa vyama katika kuunda umoja wa kitaifa kuachiwe chama kilichoshinda kuchagua, kutokana na kutofautiana katika sera na ilani katika kuleta maendeleo.
Wakizungumzia kuhusiana na suala la kuinua uchumi na kukuza ajira viongozi hao wametaja mikakati ikiwemo kutunga sera nzuri katika usimamizi wa mafuta na gesi pamoja na kutoa ajira na kulipa mishahara kutokana na taaluma na majukumu ya kazi.
Mdahalo huo uliwaalika vyama mbalimbali ikiwemo Chama cha Mapinduzi CCM, Chama cha wananchi CUF, TLP, Na vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA ambao hawakuweza kuhudhuria katika mdahalo huo.