Ijumaa , 18th Sep , 2015

Dirisha la usajili la Timu shiriki za ligi ya mpira wa kikapu mkoa wa Dar es salaam limefunguliwa rasmi huku likitarajiwa kufungwa wiki mbili baada ya kuanza michuano hiyo Oktoba mbili uwanja wa ndani wa taifa jijini Das es salaam.

Rais wa Mpira wa Kikapu mkoa wa Dar es salaam Mwenze Kabinda amesema, ligi ya Mkoa inatarajia kushirikisha timu 12 za wavulana na sita za wasichana ambapo tayari zipo kwenye maandalizi.

Mwenze amesema, uongozi kwa ujumla unaendelea na maandalizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusaka wadhamini watakaosaidia kufanikisha ligi hiyo.