Ijumaa , 18th Sep , 2015

Baada ya msanii wa muziki wa kike anayekuja kwa kasi, Lolo Da Princess amefafanua ujumbe mzima ambao unabebwa na
project yake mpya inayokwenda kwa jina 'Mishale' akiwa amefunika kidogo ujumbe halisi alionuia kuufikisha kwa kutumia usanii wake.

Diva wa kike nchini ambaye ni msanii wa muziki na muigizaji filamu Zuhura aka Lolo Da Princess

Lolo ameiambia eNewz kuwa, Mishale ni neno ambalo lina tafsiri mbalimbali kwa sasa, akifafanua kuwa kazi hiyo mpya iliyopokelewa vyema na mashabiki ni kuhusiana na suala la kutunza muda.