Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura,
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa TMF Ernest Sungura wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya kuboreshwa kwa mfuko huo toka kuwa Mfuko wa Vyombo Habari Tanzani na kuwa Taasisi ya Vyombo vya Habari.
Sungura ameongeza kuwa vyombo vingi vya habari hapa nchini huandika habari za mijini na wanasiasa zaidi na kuacha kuandika habari za vijijini kwenye watu wengi wenye matatizo na changamoto nyingi.
Aidha Sungura ameongeza kuwa pamoja na kubadilika kwa jina lakini kazi zao zitakuwa ni zile zile za kufadhili vyombo vya habari na waandishi kufanya habari za uchunguzi na zenye kugusa watu wa chini na safari hii imeongeza vipengele vipya.