Alhamisi , 3rd Sep , 2015

Baada ya kimya cha muda mrefu kwa upande wa muziki, Rich Mavocal ameibuka na kukanusha kurudishwa nyuma kimuziki kutokana na kushikiliwa chini kimapenzi na kusema kuwa ana kazi kibao ambazo zipo akiwa anasoma wakati sahihi wa kuziachia.

Rich Mavocal

Mavocal ambaye anajipanga kwaajili ya kurudi tena mwishoni mwa mwezi wa 10 ama mwanzo wa mwezi wa 11, akieleza pia pembeni ya muziki kuna biashara nyingine ambazo anafanya, baadhi ya mambo kuvurugika katika game ikiwa pia ni sababu ya ukimya wa mkali huyo.

Kuhusiana na msimamo wake kisiasa ambao upo wazi, akiwa anasapoti CCM, Rich amesema kuwa ameamua kusimama upande huo kutokana na chama hicho kumlea na kuwa pia ni chama cha familia yake nzima.

Rich Mavical hapa anazungumzia ukimya wake;