Alhamisi , 3rd Sep , 2015

Waamuzi wanaotarajiwa kuchezesha mechi ya kuwania kufuzu fainali za AFCON kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania na Nigeria wanatarajkiwa kuwasili hii leo kwa ajili ya maandalizi ya mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa Jumamosi ya wiki hii uwanja wa Taifa.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Baraka Kizuguto amesema, waamuzi hao ambao ni mwamuzi wa kati, mwamuzi msaidizi na mwamuzi wa akiba wote wanatoka nchini Rwanda huku kamisaa wa mchezo huo akiwa anatokea nchini Uganda wote watawasili nchini hii leo kw aajili ya mchezo huo wa Jumamosi.

Kizuguto amewataja waamuzi hao kuwa ni Louis Hakizimana ambaye ni mwamuzi wa kati huku Honore Simba akiwa mwamuzi msaidizi na Jean Bosco Nivitegeka akiwa ni mwamuzi msaidizi na Abdoul Karim Twagiramukiza akiwa ni mwamuzi wa akiba ambapo kamisaa ni Charles Kasembe.

Kizuguto amesema, kwa upande wa ulinzi na usalama, Jeshi la Polisi nchini likihakikisha kuwa na ulinzi wa kutosha kwa washiriki watakaoingia na kutoka uwanjani.