Akizungumza na East Africa Radio kutoka nchini Uturuki Mkwasa amesema hali wanaendelea na mazoezi isipokuwa mchezaji Abdi banda ni majeruhi lakini wachezaji wengine wanajiandaa kwa kila hali ili kujisogeza katika nafasi za juu katika nafasi ya FIFA.
Mkwasa amesema, wachezaji wote wamejiandaa vizuri na mechi ya kesho ya kirafiki dhidi ya Libya ambayo itawafanya wajiweke vizuri zaidi kwa ajili ya mechi dhidi ya Nigeria Septemba tani Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Kwa upande wake, Kocha wa Magoli kipa Peter Manyika amesema mazingira hapo awali yalikuwa magumu kwa magolikipa kutokana na hali ya hewa lakini hivi sasa wapo vizuri na wanaendelea na mazoezi.





