Jumatano , 26th Mar , 2014

Kundi maarufu la Muziki kutoka Afrika Kusini, Mafikizolo linatarajiwa kudondosha burudani ya aina yake itakayoacha gumzo Jijini Dar es Salaam, katika ukumbi wa Mlimani City tarehe 5 mwezi Aprili mwaka huu.

Mafikizolo ambayo inaundwa na wakali Theo Kgosinkwe na Nhlanhla Nciza tayari wamejipanga vilivyo kwa ajili ya kulishambulia jukwaa katika onyesho ambalo linakuwa ni la kwanza kabisa kulifanya haba Bongo katika historia ya kundi hili.

Tiketi za onyesho hili linalosubiriwa kwa hamu, zinapatikana kwa shilingi 20,000 tu katika maeneo na mlangoni siku ya tukio, tiketi hizi zitapatikana kwa shilingi 35,000.