Jumapili , 16th Aug , 2015

Msafara wa watu 10 wa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania mchezo wa tenisi kwa walemavu wheel chair tennis kikiwa na wachezaji 9 na kocha mmoja kinaondoka Alfajili ya jumatatu kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya kikiwa na matumaini makubwa

Wachezaji wa timu ya walemavu wa Tanzania wakijifua jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho cha timu ya taifa ya tenisi ya walemavu ya Tanzania ambacho kilikuwa kikijifua katika viwanja vya tenini vya klabu ya Dar es Salaam Gymkhana kinataraji kuondoka nchi alfajili ya jjumatatu kwa njia ya barabara [usafiri wa basi] kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya ambako inakwenda kutetea taji lake la michuano ya ubingwa michuano ya wazi ya kimataifa ya Nairobi itakayoanza Agasti 19 mwaka huu.

Kocha mkuu wa kikosi hicho ambacho kinajumuisha wachezaji wa kike na wakiume Riziki Salum pamoja na manahodha wa timu hiyo Juma Nade naLucy Shirima wamesema wanakwenda huko kushindana na kupata ushindi pamoja na kukabiliwa na changamoto kubwa ya uchakavu wa vifaa ambavyo watavitumia katika michuano hiyo.

Aidha pamoja na hali hiyo timu hiyo imezidi kuwaomba Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kuiunga mkono timu hiyo ambayo inahistoria nzuri katika ushiriki wake michuano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo ya dunia iliyofanyika nchini Afrika kusini na timu hiyo kutwaa ushindi wa pili wa ujumla na pia kutwaa ushindi wa kwanza kwa ujumla katika michuano mikubwa ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Miongoni mwa mahitaji muhimu kwa wachezaji hao ukiondoa suala la posho za nauli na kujikimu kocha mkuu wa timu hiyo amesema Vifaa kama baiskeli [wheel chairs] ambazo ndio kama miguu ya wachezaji hao wakati wa mchezo pamoja na raketi za kupigia mipira ni moja ya changamoto kubwa sana katika maandalizi yao [mazoezi] na hata katika mashindano yenyewe kwa ujumla.