Jumatano , 12th Aug , 2015

Kocha Mkuu wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, amesema kuwa, sasa kikosi chake kinakabiliwa na tatizo moja la mshambuliaji pekee ambalo yupo mbioni kulitatua kabla ya kuanza kwa ligi kuu.

Katika taarifa yake, Kerr amesema kikosi chake kinaundwa na washambuliaji watatu tu wa kati ambao ni Mussa Hassan Mgosi, Ibrahim Ajibu pamoja na Mganda, Hamis Kiiza aliyejiunga hivi karibuni, huku Elias Maguli akiwekwa pembeni.

Kerr amesema, mpaka sasa mawazo yake yote anayaelekeza katika kuwinda saini ya mshambuliaji wa kati ambaye atakuja kuongeza nguvu katika kikosi hicho ikiwa ni maandalizi ya msimu ujao.

Kerr amesema anaamini wakifanikiwa kupata saini ya mshambuliaji atakayekuja itakuwa ndiyo mwisho wa kufanya usajili kwa sasa ndani ya timu hiyo na anaamini watakuwa tayari kwa ajili ya kuanza harakati za kupigania Ubingwa.